Huwezi kusikiliza tena

Komla:Rambi Rambi kutoka TZ

Watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa maeneo mbalimbali duniani ambao Mwandishi wa BBC aliyeaga dunia wiki moja iliyopita, Komla Dumor, aliwahoji katika shughuli zake za uandishi wameendelea kutoa pole zao kutokana na kifo cha Komla.

Katibu mkuu kiongozi nchini Tanzania, Balozi Ombeni Sifue, naye katika kikao na waandishi wa habari, alielezea namna anavyomkumbuka mwandishi huyo Komla Dumor.