Maelfu ya walemavu wadai haki India

Haki miliki ya picha AP

Maelfu ya watu walemavu Nchini India wameandamana katika mji mkuu wa Taifa hilo New Delhi, kushinikiza Bunge la taifa hilo kupitisha mswaada unaosubiriwa kwa muda mrefu, wa kuwapa haki sawa ya kupata elimu na ajira.

Baadhi yao walibeba mabango yenye maandishi 'tunataka haki zetu, sio msaada wenu.'

Mswaada huo unatarajiwa kuwasilishwa Bungeni wakati wa vikao vya sasa hatimaye juma hili.

Inakisiwa kuwa India ina kati ya watu walemavu wapatao milioni 40 hadi milioni tisini.

Wakereketwa wanasema kuwa walemavu ni baadhi ya watu wanaotengwa zaidi na wanachukuliwa kama mzigo na jamii zao hasa katika maeneo ya vijijini.