Huwezi kusikiliza tena

Wazee maskini kusaidiwa Kenya

Serikali ya Kenya imesema kuwa itawapatia wazee masikini dola 24 kila mmoja kwa mwezi katika juhudi za kupunguza umasikini nchini humo.

Wizara ya leba na ustawi wa jamii nchini humo inasema hatua hii ni juhudi za mwanzo katika kupunguza umasikini na kupunguza mzigo kwa familia, ambazo zimekua zikiwalea wazee wasiojiweza na hasa masikini hohe hahe.

Mwandishi wa BBC Ng'endo Angela amezungumza na Waziri wa Leba na ustawi wa jamii Kenya, Kazungu Kambi na kwanza anaelezea vigezo vilivyotumiwa kuwatambua masikini hawa.