Huwezi kusikiliza tena

Mafao yaleta kero Tanzania

Kumekuwa na malalamiko nchini Tanzania kuhusiana na wabunge nchini humo kujiongezea mafao ya takriban dola za Marekani laki moja.

Wakazi wa Dar es Salaam wameiambia BBC wameshtushwa na hatua ya wabunge kujiongezea mafao hasa baada ya kuwepo kwa taarifa serikali haina fedha za kutumia kwa huduma za kijamii.

Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam Aboubakar Famau ana taarifa zaidi.