Huwezi kusikiliza tena

Ghana yajikita katika mimea ya GMO

Masuala machache yameleta mgongano wa kimaoni katika ulimwengu wa ukulima kuhusiana na mimea inayokuzwa na vinasaba au GMO. Kama vyakula vilivyokuzwa kwa njia ya kisayansi,mbali na kukabiliana na uhaba wa chakula kwa wengine ,vyakula vilivyokuzwa na vinasaba kwa mara nyingi huonekana kuwa hatari dhidi ya mazingira na kwa upande mwengine vikawa suluhu ya baa la njaa kwa idadi kuu ya watu kutokana na upungufu wa mazao.