Huwezi kusikiliza tena

Uhuru wa biashara ni ndoto au?

Uchumi ndio uti wa mgongo wa jumuiya ya Arika Mashariki. Biashara huria, hususan sekta binafsi, ni kiungo kikuu na muhimu sana.

Taasisi kadha zimeundwa na kuzatitiwa ili kuiwezesha na kuirahisisha, - soko moja, forodha moja na mfumo mmoja wa fedha.

Hata baadhi ya vizuizi vya vibali na barabarani vinang'olewa ili mitaji na nguvukazi zisambae kwa urahisi.

Lakini je, biashara kati ya nchi wanachama ni huru kama inavyodaiwa au bado ni ndoto? Kutujibia swali hili, mwandishi wa BBC wa maswala ya uchumi, Alli Mutasa anatathmini kutoka Kampala: