Huwezi kusikiliza tena

Jifahamishe Olimpiki majira ya baridi

Mashindano ya Olimpiki ya majira ya baridi yanaanza rasmi hivi leo katika mji wa Sochi nchini Urusi huku usalama ukidumishwa.

Naibu waziri mkuu wa Urusi Arkady Dvorkovich ameiambia BBC kwamba zaindi ya wanajeshi alfu arobaini, polisi na maafisa wengine wa usalama wametumwa kushika doria wakati wa mashindano hayo.

Viongozi kadhaa wa dunia wanahudhuria sherehe za ufunguzi wa mashindano hayo. Yametajwa kuwa mashindano yatakayokuwa na gharama ya juu zaidi kuandalia. Je unaelewa vipi mashindano haya ya Olimpiki majira ya baridi?