Huwezi kusikiliza tena

Hatari kwa usalama wa Ndovu

Mkutano wa kimataifa kuhusu masilahi ya wanyamapori, ulifanyika mjini London siku ya Alhamisi.

Kongamano hilo lilidhamiria kutafuta mbinu ya kulinda wanyamapori walio katika hatari ya kuangamia.

Miongoni mwa wanyama wanaokabiliwa na hatari hiyo ni Ndovu ambao huuliwa kwa melfu na wawindaji haramu wakitafuta pembe zao.

Hitaji la pembe hizo liko juu sana na linachochewa na wafanyabiashara nchini China kama inavyoeleza taarifa hii.