Huwezi kusikiliza tena

Ukatili wazi wazi CAR

Katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Waislamu wengi wanatoroka makao yao kutokana na hofu ya vita dhidi yao.

Mashambulizi hayo yanatekelezwa na wanamgambo wa kikristo wajulikanao kama kundi la anti-Balaka, ambao wanasema kuwa wanalipiza uhalifu uliotekelezwa dhidi ya jamii yao na wanamgambo wa Kislamu.

Lakini ni raia, na sio wanamgambo ambao wanaathirika zaidi na ulipizaji kisasi huo licha ya majaribio ya viongozi wa eneo hilo kuzuia mapambano kati ya waislamu na wakristo.

Katika kijiji cha Boubua kilichoko magharibi mwa mji mkuu, Bangui, mapigano yanawalenga hata wale ambao wamejaribu kuzuia vita dhidi ya jamii zao vile mwandishi wetu wa BBC, eneo la Afrika, aligundua.