Huwezi kusikiliza tena

Ukraine hali sio hali-22 wauawa

Angalau watu 22 wameuawa katika ghasia zilizozuka upya kati ya waandamanaji na polisi mjini Kiev Ukraine, baada ya makubaliano yaliyofikiwa kutibuka.

Watu nchini humo waelezea kujionea mabomu ya petroli , risasi na maji ikitumiwa katika kitovu cha maandamano, medai ya uhuru.

Mkutano kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa Muungano wa Ulaya na Rais Yanukovych yanaendelea. Hata hivyo taarifa hizi ni kinyume na taarifa za awali kuwa maafisa hao walikuwa wamerejea makwao baada ya mazungumzo kukosa kufanyika.

Muungano wa Ulaya unatarajiwa kujadili swala la vikwao baadaye.

Walioshuhudia ghasia hizo wanasema kuwa karibu watu 21 na 27 wameuawa.

Polisi mmoja ameripotiwa kuuawa.