Huwezi kusikiliza tena

Nipe nikupe ya Samaki na Ngono Kenya

Inakadiriwa takriban watu milioni moja na nusu wanaishi na virusi vya HIV na maradhi ya UKIMWI nchini Kenya.

Wavuvi vijijini huwapa wauza samaki wanawake samaki kama malipo kwa kufanya nao ngono badala ya pesa.

Lakini sasa mashirika ya misaada yanajaribu kubadilisha tabia hii, ijulikanayo kama 'kubadilisha ngono na samaki'.

Wanawahimiza wanawake wanunue mashua zao wenyewe. Mariam Omar ana zaidi toka magharibi mwa Kenya.