Huwezi kusikiliza tena

Waisilamu watoroka mashambulizi CAR

Zaidi ya wakimbizi elfu mbili Waislamu kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati wamefika Cameroon baada ya kukimbia mzozo wa kidini unaoendelea nchini mwao.

Mzozo ulianza baada ya waasi, wengi wao Waislamu wa kundi la Seleka kuchukua usukani wa madaraka na baadaye kuupoteza mwaka jana. Kilichofuata ni kulipiza kisasi dhidi ya Waislamu wote.

Na njia pekee ya kukimbia salama ni kwa msafara wa muungano wa Afrika, MISCA, mara moja kila mwezi. Mwandishi wetu kassim Kayira ameambatana na msafara huo.