Huwezi kusikiliza tena

Vifo vya watoto vingali vingi

Saa ishirini na nne za kwanza za maisha ya mtoto ni muhimu na ni za hatari sana, wengi sana hufa katika siku ya kwanza tangu wanapozaliwa.

Shirika la misaada kwa watoto la Save the Chidlren limechapisha hivi karibuni taarifa inayobainisha ukubwa wa tatizo na njia za kuzuia.

Zifuatazo ni baadhi ya hadidu muhimu kutoka taarifa yao kote duniani, watoto milioni moja hufariki dunia kila mwaka, siku ya kwanza, mara baada ya kuzaliwa.

Save the Children, linaamini vifo hivi vingi vinazuilika iwapo watu wangekuwa na uwezo wa kuhudumiwa na watabibu wenye ujuzi. Pakistan, India na Nigeria, ni kati ya mataifa yenye idadi kubwa ya watoto wachanga wanaozaliwa tayari wamekufa.

Nigeria inaongoza barani Afrika kwa vifo vya watoto aina hiyo.

Vifo vingi vya watoto pia hutokea Sudan Kusini, huku maelfu ya watu wakikimbia makazi yao - takriban watoto wachanga elfu tano hufariki dunia siku ya kuzaliwa kila mwaka nchini humo.

Anne Soy yupo mjini Nimule Sudan Kusini mpakani na Uganda.