Huwezi kusikiliza tena

Njaa na masaibu mengine Turkana

Kaunti ya Turkana kaskazini mwa Kenya inakabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika miaka ya karibuni.

Takriban watu milioni moja kutoka Kaskazini mwa Kenya wanahitaji msaada wa chakula cha dharura.

Wabunge wa eneo hilo wanaonya huenda watu wengi zaidi wakafariki dunia iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa.

Ukame umetokea licha ya serikali kutangaza kupatikana kwa viwango vikubwa vya maji eneo hilo, vinavyoweza kutosheleza nchi nzima kwa miaka sabini ijayo.

Mwandishi wetu Emmanuel Igunza anaripoti kutoka Turkana.