Huwezi kusikiliza tena

Wahamiaji wanavyopenya kuingia Hispania

Polisi wa Hispania wametoa video inayoonyesha mamia ya wahamiaji wakivuka isivyo halali katika mji mdogo wa Mel-eelya.

Hispania inasema takriban wahamiaji elfu moja wameweza kuingia mji huo, ikiwa ndio idadi kubwa zaidi kuvuka katika miaka kumi iliyopita.

Mwezi uliopita Jumuia ya Ulaya ililaumu polisi wa nchi hiyo kutumia risasi ya mpira kuwazuia wahamiaji waliokua wameulenga mji mwengine wa Hispania, Ceuta. Kassim Kayira anaeleza.