Huwezi kusikiliza tena

Kifua Kikuu hatari kwa vijana TZ

Leo ni siku ya kimataifa ya kifua kikuu!

Ugonjwa huo umeendelea kuwa janga la kiafya duniani na ni miongoni mwa magonjwa ya kuambukiza yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya watu.

Ni ugonjwa wa pili baada ya Ukimwi.

Kifua Kikuu pia unajulikana kama ugonjwa wa maskini, ukiathiri kundi kubwa la vijana ambao ni nguvu kazi.

Katika idadi ya mamilioni ya watu wanaougua ugonjwa wa kifua kikuu duniani, robo tatu wanatoka barani Afrika, Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi hizo, ambapo wagonjwa 64 elfu huandikishwa kila mwaka nchini humo.

Ben Mwang'onda kutoka Dar es Salaam anaarifu zaidi