Huwezi kusikiliza tena

Juhudi za kumuokoa mtoto

Mtoto aliyejeruhiwa na risasi iliyomuua mama yake katika shambulio lililofanywa kwenye kanisa la JOY OF JESUS Likoni Mombasa Nchini Kenya jumapili amefikishwa jijini Nairobi kwa Ndege .

Satrin Osinya mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa katika Hospitali kuu ya Kitaifa ya Kenyatta ili kuondoa risasi iliyoingia kwenye ubongo wake baada ya kumuua mama yake .