Huwezi kusikiliza tena

Wanawake wamechangia vipi amani?

Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira{UNEP} linazindua ripoti yake hii leo kuhusu mchango wa wanawake katika maeneo ya vita na usimamizi wa mazingira.

Ripoti hii imetayarishwa na mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa yakiangazia mataifa ya Uganda, Sudan Kusini, Sierra leone miongoni mwa mengine.

Nchini kenya ni miaka miwili tangu kuzuka machafuko ya kijamii ukanda wa Tana.

Familia nyingi hususan wanawake wamekua na changamoto kujaribu kurejelea maisha ya kawaida. Mwandishi wa BBC Patience Nyange alitembelea eneo hilo na kuandaa taarifa hii.