Huwezi kusikiliza tena

KDF itaendelea kuwepo Somalia

Tangu Jeshi la Kenya liivamie Somalia Kusini, mwaka wa 2011, wapiganaji wa kiislamu la Al Shabaab wamezidisha mashambulizi yake nchini Kenya.Licha ya uvamizi huo wenye maafa makubwa kwa raia, Brigedia George Owino anayeoongoza kikosi cha wanajeshi wa Kenya, KDF nchini humo, anasema hawatoki Somalia wakati wowote karibuni hadi wahakikishe wameikomboa Somalia nzima. Katika mazungumzo yake na John Nene, Brigedia Owino amekanusha uvamizi wa Al Shaabab Kenya, kutokana na uwepo wa KDF Somalia.