Huwezi kusikiliza tena

Vita dhidi ya Al Shabaab

Majeshi ya Umoja wa Afrika ya Kulinda amani nchini Somalia yameshambuiwa na bomu la kutegwa kando ya barabara katika mji wa Kismayo.

Hii ni moja tu ya mfululizo wa mashambulio dhidi yao ambayo mpaka sasa yamesababisha vifo vya zaidi ya wanajeshi elfu mbili wa Amisom.

Na kwa sasa Juhudi mpya za kupambana na Al-Qaeda na washirika wake zimeanzishwa, zikianzia Afrika. Vikosi vya mataifa ya Afrika, vikiongozwa na Muungano wa Afrika, ndivyo vinaendeleza mapambano hayo.

Katika mji wa Korioli, nchini Somalia, wanajeshi wa Uganda wanaviongoza vikosi vinavyopambana na Al Shabaab.

Kuna zaidi ya wanajeshi elfu sita wa Uganda nchini Somalia, na zaidi ya elfu mbili na mia saba wamekufa wakiwa vitani.

Al Shabab bado wanayadhibiti maeneo kadha nchini Somalia.