Kenya yaruhusu waandishi katika uwanja wa Kasarani
Huwezi kusikiliza tena

Kenya yawarejesha nyumbani wakimbizi

Kwa mara ya kwanza tangu polisi walipoanza operesheni nchini Kenya, waandishi wa habari wamekubaliwa kuzuru uwanja wa kasarani unaoshikilia watu zaidi ya mia moja katika wale mia nne khamsini wanaoshikiliwa.

Idara za usalama nchini humo zinasema watu hao bado wanashikiliwa huku wakiendelea kuchunguzwa.

Mapema leo hii, wasomali themanini na wawili waliokua nchini Kenya kinyume na sheria wamerejeshwa Somalia.

Zaidi ya watu elfu tatu walikamatwa katika operesheni hii ambayo watetezi wa haki za binadamu wameshitumu kwa kukiuka haki za binadamu.

Robert Kiptoo anaarifu zaidi.