Nyumba ya watuhumiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda
Huwezi kusikiliza tena

Makao ya watuhumiwa wa mauaji Rwanda

Kufuatia mauaji ya kimbari ya mwaka 94 nchini Rwanda, Umoja wa Mataifa uliunda mahakama maalum ya kuwashtaki washukiwa wa mauaji hayo, makao yake yakiwa mjini Arusha Tanzania.

Miongoni mwa washukiwa kulikuwa na watu kumi na wanne, maafisa wa wakuu wa zamani katika serikali, ambao hawakukutwa na hatia, lakini hawana pa kwenda.

Wanaogopa kwenda Rwanda, na hawawezi kuhamia nchi nyingine.

Anne Soy amewatembelea mjini Arusha na kuandaa taarifa hii.