Huwezi kusikiliza tena

Athari za mauaji ya kimbari ni wazi DRC

Miaka 20 baada ya mauaji ya kimbari ya Rwanda, bado madhara yake yanaonekana katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Hii ni kwa sababu Wahutu wengi waliokimbia Rwanda walikwenda huko.

Baadhi ni wakimbizi, lakini wengine wanatuhumiwa kushiriki katika mauaji kama wapiganaji wa FDLR.

Na huku wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na wale wa Kongo wakijiandaa kushambulia FDLR, mwandishi wetu Lubunga ByaOmbe ametutumia taarifa ifuatayo kutoka Mashariki mwa Congo.