Huwezi kusikiliza tena

Watu 2 wanaoleta amani CAR

Ni nchi iliyosambaratishwa kabisa na ghasia za wenyewe kwa wenyewe.

Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia kwenye ghasia mwaka mmoja uliopita, baada ya serikali kupinduliwa na wapiganaji wa kiislamu wa Seleka.

Baadae na wao walianza kuvamiwa wa wapiganaji wa Kikristo,

Vurugu hizo zimeshuhudia maelfu wakiuawa na wengine wengi wakikimbia nchi hiyo.

Sasa waleta amani wawili wamedhamiria kuleta maridhiano, mmoja Muislam na mwengine Mkristo.

Zuhura Yunus anaarifu zaidi.