Huwezi kusikiliza tena

Tatizo la Dawa bandia TZ

Kero la kuzagaa kwa dawa bandia nchini Tanzania ni hai, na kikubwa ni kwamba nyingi ya dawa hizo ni zile zinazotumiwa kutibu ugonjwa wa Malaria.

Changamoto hapa ni kwamba mamilioni ya watanzania huugua ugonjwa huu kila mwaka huku maelfu wakifariki.Wapate wapi tiba?

Je ulijua kama wafanyabiashara wanaoiona hali hii kama pengo la kibiashara na nafasi kwao kuuza dawa bandia?

Wiki hii Haba na Haba inaangazia tatizo la uwepo wa dawa bandia na changamoto inayotokana na hali hiyo kwa wagonjwa

Msimulizi wako ni Claudia Mayanka