Huwezi kusikiliza tena

Mkaa kutoka kwa takataka Burundi

Mradi mpya wa kutumia takataka kutengeneza mkaa umesifiwa kwa kusaidia kuhifadhi mazingira nchini Burundi.

Kumekuwa na tishio dhidi ya misitu nchini humo kutokana na kuongezeka kwa ukataji haramu wa miti inayochomwa kutengeneza mkaa.

Shirika moja la vijana nchini Burundi, limetuzwa kwa jitihada zake za kulinda mazingira, katika hali ambayo wataalamu wanasema tani moja ya mkaa inaweza kunusuru ekari moja ya msitu.

Mwandishi wetu wa Bujumbura Ismail Misigaro ametembelea kiwanda kidogo cha utenegenzaji mkaa huo na hii hapa taarifa yake.