Huwezi kusikiliza tena

Mauaji ya kikatili yaendelea Syria

Wakati vita vilivyojaa ukatili vikiendelea nchini Syria, katika mji kubwa wa Aleppo, maelfu ya watu imearifiwa wameuawa au kujeruhiwa kutokana na mabomu yanayoporomoshwa kutoka angani mwaka huu.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeyashutumu majeshi ya Rais Assad kwa ukatili katika jiji la Aleppo dhidi ya raia, kutokana na mabomu yanayoporomoshwa na helikopta kutoka futi 7000 .

Waandishi wa BBC walipata fursa ya pekee kuuzunguka mji huo kwa siku nne, kama Zuhura Yunus anavyotuarifu.