Huwezi kusikiliza tena

Midahalo ya misaada Malawi

Ikiwa ni moja ya nchi masikini sana duniani, Malawi inategemea sana misaada.

Lakini uhusiano wake na mataifa yanayotoa misaada ni wa mashaka na msaada wa kifedha umesimamishwa mara nyingi kutokana na Malawi kukiuka haki za binadamu na kukithiri kwa rushwa.

Kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 20, BARUAN MUHUZA anaangazia namna midahalo kuhusiana na misaada ilivyotawala siasa za Malawi.