Huwezi kusikiliza tena

Mtego wa ukahaba wanasa watoto Malindi

Watoto wa kike wenye hadi umri wa miaka kumi na miwili, wanalaghaiwa na kuchagizwa kuingia katika ukahaba.

Katika mji unaoonekana kama peponi, Malindi uliopo kwenye pwani ya Kenya, kisirisiri unaendesha biashara ya ngono kwa watoto.

Watalii huwa tayari kulipa fedha ili kufanya ngono katika maeneo ya mwambao.

Mwandishi wetu Anne Soy yuko Malindi na tunaungana naye moja kwa moja. Tatizo hili la watoto kuingia katika ngono na watu wazima hasa watalii limeenea kiasi gani- Anne