Huwezi kusikiliza tena

Nyota wa 'Bongo Movie' watembelea BBC

Bongo movie kama inavyojulikana sasa nchini Tanzania inazidi kushamiri kadri miaka inavyozidi kwenda.

Filamu hizo zinaozigizwa kwa lugha ya Kiswahili hutazamwa na wazungumzaji wa lugha hiyo ndani na nje ya Tanzania.

Lakini suala kubwa la kujiuliza ni iwapo waigizaji wa filamu hizi wanafaidika. Leo tumetembelewa na mabinti wawili, wote wakiwa waigizaji maarufu nchini humo, Riyama Ali na Wastara Juma.

Waigizaji hawa wamekuja hapa Uingereza kutengeneza filamu inayoitwa 'Ughaibuni.'

Kwanza Kasim Kayira amezungumza na Wastara Juma,akianza kwa kumuuliza changamoto wanazokumbana nazo kama wasanii.