Huwezi kusikiliza tena

Matumaini ya chanjo ya malaria

Wanasayansi wa Marekani wanasema wamepiga hatua katika kutafuta chanjo dhidi ya malaria.

Watafiti walifanya uchunguzi wao nchini Tanzania ambako walipata watoto wenye kinga ya kimaumbile dhidi ya malaria.

Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida liitwalo Journal Science, uligundua kuwa miili ya watoto hao hutoa kinga, yaani antibody, ambayo inashambulia vidudu vya malaria, vinavoambukizwa na mbu.

Wana-sayansi wanasema majaribio zaidi yanahitajika kufanywa kwa wanyama na binaadamu, kujua hasa kama chango hiyo kweli tafanya kazi

Mwandishi wa BBC John Solombi na maelezo zaidi