Huwezi kusikiliza tena

David Rudisha kurejea uwanjani

Bingwa wa michezo ya Olympiki mbio za mita mia nane David Rudisha wa Kenya ametangaza rasmi anarudi uwanjani Mei tarehe 31 mwezi huu katika mbio za Golden League huko Oregon, Marekani, baada ya kutokimbia kwa muda wa mwaka mmoja akiuguza jeraha la goti la kulia.

Rudisha, ambaye pia anashikilia rekodi ya dunia, amezungumza na John Nene huko Iten eneo la bonde la ufa wakiwa mazoezini pamoja na kusema sasa yuko sawa na tayari kukimbia tena.