Huwezi kusikiliza tena

Chai afueni ya umasikini Sudan

Nchini Sudan, maelfu ya wanawake waliokimbia vita Darfur na Kordofan ya Kusini wanajikimu kimaisha kwa kuuza chai katika barabara za mji mkuu wa Sudan Khartoum.

Wanawake hawa wanafanya biashara zao kando kando ya barabara, katika bostani na katika masoko.

Lakini serikali ambayo inakabiliana na biashara ambazo hazijasajiliwa na mashindano kutoka kwa wakimbizi wa Ethiopia na Eritrea,kina mama hawa wauza chai kwa sasa wanakabiliwa na changamoto kubwa.

Mariam Omar anaarifu zaidi.