Kishawishi cha Kenya kwa watalii

Kenya imetangaza vivutio kadhaa ili kuvutia watalii zaidi - wa ndani na wa nje - nchini humo, ikiwemo bei nafuu ya kutembelea mbuga za wanyama, na hata kuteremsha nauli za ndege.

Sekta ya utalii nchini Kenya inakabiliwa na hasara kubwa kutokana na kutetereka kwa hali ya usalama.

Katika miaka mitatu iliyopita, kumekuwa na ongezeko la mashambulio yanayohusishwa na kundi la Al Shabaab.

Mwandishi wa BBC mjini Nairobi Anne Soy anasimulia taarifa hiyo.