Huwezi kusikiliza tena

Mtanzania ahamasisha dunia

Hebu tafakari, kusafiri kutoka nchini Chile Amerika ya Kusini hadi London na kisha kuvuka mpaka na kuingia Ujerumani na kisha kwenda Afrika?

Kwa wanaotumia ndege, safari hiyo sio hoja.

Lakini kwa mwanamume mmoja mtanzania, Lelo Elvis Munis, safari yake imemchukua zaidi ya miaka miwili ingawa kwa manufaa na faida ya jamii.

Lelo Elvis Munis, amekuwa akiendesha baisikeli kote duniani kwa lengo la kuhamasisha Afrika kuhusu uhifadhi wa mazingira na kuchangisha pesa kuwasaidia vijana wa Tanzania kupata elimu muhimu wanayoihitaji. Amekuwa akisafiri kwa karibu miaka miwili na anakaribia kumalizia safari yake wiki ijayo katika eneo la Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania.

Mwandishi wa BBC Robert Kiptoo, alikutana na Elvis mjini Nairobi baada ya kuwasili kutoka Rwanda