Huwezi kusikiliza tena

Historia ya kombe la dunia

Alhamisi ijayo michuano ya kombe la dunia inaanza rasmi nchini Brazil na tayari mihemko imeanza kushuhudiwa miongoni mwa mashabiki wa timu za mataifa yatakayoshiriki kindumbwendumbwe hicho.

Kama sehemu ya maandalizi ya matangazo ya kipute hicho hapa BBC leo tunaanza kukuletea makala maalum ya kombe la dunia nchini Brazil na ni zamu ya Eric David Nampesya na historia fupi ya michuano hiyo.