Huwezi kusikiliza tena

Ujangili wakithiri Kenya

Mamlaka ya Kenya imekamata pembe za tembo zinazoaminika zimetoka kwa tembo wasiopungua 114, na kufanya operesheni hii kuwa ndio iliyofanikiwa zaidi mwaka huu baada ya kugundua pembe nyingi zaidi.

Washukiwa walikamatwa katika eneo moja la bandari ya Mombasa, Maafisa wanasema kuwa pembe hizo huenda zimetoka sehemu mbalimbali za Afrika , na tukisalia na hilo nchini Tanzania serikali bado ina kibarua kigumu kukomesha biashara hii haramu ya pembe za tembo kama anavyotuarifu Aboubakar Famau .