Huwezi kusikiliza tena

Kero la ubakaji Sudan Kusini

Viongozi wa kimataifa wanakutana jijini London kuanzia hii leo, kwa kongamano kuhusu kumaliza dhulma za kimapenzi katika mataifa yanayokabiliwa na mizozo.

Mkutano huo, wa siku nne umeandaliwa na Waziri wa masuala ya nchi za kigeni wa Uingereza, William Hague.

Mkutano huo umeandaliwa huku mataifa kadhaa barani Afrika yakikabiliwa na changamoto ya kumaliza ubakaji unaotumiwa kama silaha ya kivita.

Mwandishi wetu Emmanuel Igunza, amekuwa nchini Sudan Kusini kuchunguza jinsi mzozo unaoendelea nchini humo, umechangia pakubwa katika ongezeko la wanawake wengi waliobakwa katika takriban miezi sita ya mapigano.