Huwezi kusikiliza tena

Mashabiki washambuliwa ukumbini Nigeria

Takriban watu 20 wameuawa katika shambulizi lililofanywa na wapiganaji wa Boko Haram Kaskazinimwa Nigeria walipokuwa wanatazama michuano ya kombe la dunia

Takriban watu 27 wanasemekana kujeruhiwa vibaya katika mji wa Damaturu, jimbo la Yobe.

Michuano ya kombe la dunia imekuwa ikionyeshwa katika kumbi za umma nchini Nigeria ingawa katika baadhi ya maeneo imepigwa marufuku kutokana na tisho la usalama la Boko Haram.