Waandishi wa Aljazeera wafungwa
Huwezi kusikiliza tena

Waandishi wa Al Jazeera wafungwa Jela

Mahakama nchini Misri imewahukumu jela wandishi watatu wa habari wa shirika la Al Jazeera waliokuwa wamezuiliwa kwa miezi sita nchini humo.

Walipatikana na hatia ya kueneza habari za kupotosha na kushirikiana na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Muslim Brotherhood.

Mmoja wa wandishi hao ni Peter Greste, raia wa Australia na ambaye pia alikuwa mwandishi wa habari wa BBC wakati mmoja alipokea hukumu ya kifungo cha miaka saba.

Mwenzake Baher Mohamed alifungwa jela miaka kumi.

Watuhumiwa wengine kumi na moja waliohukumiwa bila ya wao kuwepo gerezani, walipokea vifungo vya miaka 10 kila mmoja.