Huwezi kusikiliza tena

Marufuku ya Miraa yaanza rasmi UK

Marufuku ya utafunaji wa miraa nchni Uingereza inaanza kutekelezwa leo na kusababisha hofu ya kupoteza ajira kwa wakulima Kenya.

Mmea wa Khat au Miraa huliwa na watu kutoka mataifa ya Ethiopia, Kenya, Somalia na Yemen.

Serikali ya Uingereza imesema kuwa hatua ya kupiga marufuku Miraa inaambatanisha nchi hiyo na mataifa ya Ulaya ambayo pia yameharamisha Miraa kwa sababu ya athari zake za kiafya.

Hata hivyo nchini Kenya , wakulima wa Miraa wana hofu kuwa hatua ya Uingereza itawakwamisha kiuchumi.