Huwezi kusikiliza tena

Mwanamke aliyeasi dini 'ameghushi' hati

Mwanamke wa Sudan aliyeachiwa huru baada ya kuhukumiwa kifo kwa madai ya kuasi dini ya kiislamu kwa kuolewa na mkristo anatuhumiwa kughushi hati za kusafiria ili kuondoka, mwanasheria wake ameiambia BBC.

Meriam Ibrahim alikamatwa siku ya Jumanne, siku moja baada ya mahakama kumwachia huru ambapo ilibatilisha hukumu yake ya kifo kutokana na kuasi imani ya kiislamu.

Mke wa Ibrahim alikuwa na hati za dharura zilizotolewa na serikali ya Sudan Kusini wakati alipokamatwa katika uwanja wa ndege wa Khartoum. Aliripotiwa kuwa alikuwa na mpango wa kwenda nchni Marekani yeye na familia.