Huwezi kusikiliza tena

Kashfa ya tiketi yakumbwa FIFA

Maafisa wa polisi nchini Brazil wamemkamata afisa mkuu mtendaji wa kampuni mshirika wa FIFA kwa tuhuma za uuzaji tiketi za kombe la dunia kinyume na kanuni.

Ray Whelan ambaye ni meneja mkuu mtendaji wa kampuni mshirika wa FIFA 'Match Hospitality' alikamatwa katika hoteli moja huko Rio de Janeiro , inayotumika pia na maafisa wa shirikisho la FIFA.

Juma lililopita watu wengine 11 walikamatwa kwa kuuza tiketi za kombe la dunia kinyume na kanuni za FIFA .

Polisi walisema kuwa kikundi hicho kilikuwa sehemu ya genge kubwa la kimataifa ambalo lilikuwa likiuza tiketi ambazo zilikuwa zimetengewa makundi maaluma ikiwemo tiketi zilizokuwa zimetengewa wachezaji .