Huwezi kusikiliza tena

Mkenya ashinda tuzo ya Caine

Mkenya Okwiri Oduor ndiye mshindi wa tuzo la Caine - inayotolewa kwa waandishi maarufu zaidi wa Kiafrika.

Tuzo hiyo ilitangazwa hapo jana Oxford Uingereza na mshindi huyo amenyakuwa zawadi ya pauni alfu kumi kwa hadithi yake 'My Father's Head'.

Hadithi hiyo ilikuwa miongoni mwa nyengine nne zilizoteuliwa kugombea tuzo hiyo.

Amesifiwa kwa kuwa mwandishi aliyetumia ustadi mkubwa kuishughulikia mada yenye majonzi makubwa.

Odeo Sirari alizungumza na Bi Okwiri Oduor muda mfupi tu baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo.

Alisema hakutarajia kuibuka mshindi.