Huwezi kusikiliza tena

Wasichana walilia uongozi bora TZ

Taasisi ya kimataifa ya MOREMI imewachagua wasichana wapatao 26 toka nchi za Afrika ambao wamekuwa katika msitari wa mbele katika harakati za kuijiimarisha kiuongozi.

Wasichana hao wapo nchini Ghana tayari kwa mafunzo maalumu ya kuwapa uwezo na mbinu za kuweza kumkomboa msichana wa Afrika.

Catherine Fidelis ni msichana wa miaka 23 kutoka Tanzania aliyechaguliwa kuwakilishi nchi hiyo kutokana na kuonekana kuwa msitari wa mbele katika harakati hizo ikiwa ni pamoja na kuanzisha Mradi ujulikanao kama Fahari ya kuwa Msichana.

Mwandishi wetu wa Dar es Salaam Leonard Mubali amefanya mahojiano na msichana kabla ya kwenda nchini Ghana na kwanza anamuuliza ni matarajio gani aliyonayo katika mafunzo hayo.