Huwezi kusikiliza tena

Mmea wa Chikanda nusura kuangamia TZ

Mmea unaojulikana kama chikanda uliopo katika hifadhi ya kitaifa ya Kitulo mkoani Njombe kusini Magharibi mwa Tanzania sasa unakabiliwa na hatari ya kuangamia.

Hi ni baada ya kuvamiwa na watu wanaoamini kuwa unatibu maradhi ya Ukimwi.

Biashara ya kuusafirisha na kuuza mmea huo imekuwa ikinoga kati ya eneo hilo na mataifa jirani ya Zambia na Malawi.

Leonard Mubali alizuru eneo na kutuandalia taarifa ifuatayo.