Huwezi kusikiliza tena

Hakuna dawa ya utajiri tena Makete

Utajiri wa mali ni hali ambayo karibu kila mtu angependa kuwa nayo ili kukidhi kikamilifu mahitaji yake. Inadaiwa kuwa nchini Tanzania baadhi ya watu kutoka maeneo tofauti hufika Makete wilaya iliyopo kusini Magharibi mwa nchi hiyo kutafuta dawa ya kupata utajiri kwa waganga wa jadi.

Hata hivyo wenyeji wa eneo hilo wanabeza imani hiyo na kudai kuwa watu wanaotoka mbali na kusafiri kwa gharama kubwa wanapoteza fedha zao tu kwani waganga wa aina hiyo hawapo.

Mwandishi wa BBC Leonard Mubali amefika eneo hilo na kutuandalia taarifa ifuatayo.