Huwezi kusikiliza tena

Ukeketaji:'Sitaki wasichana wapitie yaliyonisibu'

Hii leo wajumbe kutoka pembe mbali bali za dunia wanakongamana mjini London kujadili hatari ya Ndoa za mapema na upashaji tohara wa wasichana.

Mambo haya yamekashifiwa sana japo bado kuna baadhi ya jamii hasa barani Afrika na Asia ambapo wameshikilia utamaduni huu.

Sarah Korere ni mbunge kutoka jamii ya Samburu nchini Kenya.

Yeye mwenyewe amewahi kupitia utamaduni kama huu na kitu ambacho kimemfanya kuwa mwanaharakati wa kupinga tohara kwa wasichana.