Huwezi kusikiliza tena

Ebola yazua taharuki duniani

Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuenea kwa ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Afrika kama janga la dharura la kimataifa, ambalo linalohitaji suluhu la haraka.

Shirika hilo limesema kuwa mataifa ambayo yameadhiriwa na virusi vya ugonjwa huo hayana uwezo wa kudhibiti mlipuko huo na kuwa suala hilo linahitaji msaada wa kimataifa.

Tangazo hilo limetolewa baada ya mazungumzo ya dharura ya wataalamu wa ugonjwa huo unaoendelea mjini Geneva, kujaribu kutafuta mbinu za kuthibiti mlipuko huo, ambao umetajwa kuwa mbaya zaidi katika historia.