BBC Yazindua kituo Dar
Huwezi kusikiliza tena

BBC Yazindua kituo Dar

Ni hatua kubwa na ya kihistoria, kwa kweli sio tu kwa BBC bali pia wasikilizaji wetu wa eneo la Afrika mashariki na kati. Kiswahili kimerejea nyumbani.

Shughuli ya uzinduzi imefanya jioni hii na Mkuu wa habari wa BBC, Nikki Clarke, ambaye amekata utepe na kuwaongoza wageni waalikwa, kuweza kuzitembelea studio zetu mpya kabisa, ambazo matangazo ya Amka na BBC yatakuwa akitoka. Wageni waalikwa ni pamoja na wasiasa na maafisa wa serikali, lakini pia wapenzi na mashabiki wa BBC Idhaa ya Kiswahili. Lakini nini hasa sababu ya matangazo haya kuletwa Afrika? Zuhura Yunus ameandaa taarifa hii.